Tuesday, October 16, 2012

MAAFISA TEHAMA WA MIKOA NA HALMASHAURI WAKIWA DARASANI WAKATI WA MAFUNZO YA MFUMO WA HCMIS(LAWSON)

Maafisa Tehama mbalimbali kutoka katika Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara wakiwa katika mafunzo ya mfumo wa kiutumishi wa HCMIS (LAWSON) mjini Dodoma katika ofisi za Tamisemi.Mafunzo haya yaliendeshwa na Wizara ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 15-17/10/2012

MAAFISA TEHAMA WA MIKOA NA HALMASHAURI WAPEWA MAFUNZO JUU YA MFUMO WA HCMIS (LAWSON)

Maafisa Tehama wa sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro kulia (Kundaeli Lema) na kushoto (James Mtatifikolo) wakiwa katika mafunzo ya mfumo wa kitumishi HCMIS (LAWSON) yaliyoendeshwa na Wizara ya Utumishi wa Umma katika ofisi za Tamisemi-Dodoma  kuanzia tarehe 15-17/10/2012.Mafunzo haya yamehudhuriwa na maafisa Tehama wote wa Mikoa na Halmashauri.


Wednesday, October 10, 2012

VIONGOZI MBALIMBALI WAKIFUATILIA KWA UMAKINI TUKIO ZIMA

Viongozi wa serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe. Samwel  Sitta  na watumishi mbalimbali waliokuwepo katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wakifuatilia kwa makini tukio hilo la kihistoria katika mkoa wa Kilimanjaro.

WAKIPEANA MIKONO NA VIONGOZI WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO KATIKA UKUMBI WA MKUU WA MKOA KILIMANJARO

Wakipongezana mara baada ya kukamilisha zoezi la kusaini (Picha na Shabani Pazi)

WAKIBADILISHANA MAJALADA MARA BAADA YA KUSAINI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (Kulia) Dkt.Faisal H.H.Issa akibadilishana majalada na mwakilishi wa TIB mara baada ya kusaini 'memorandum of understanding' ya ujenzi wa soko.(Picha na Shabani Pazi)

SERIKALI YA MKOA WA KILIMANJARO YALETA MATUMAINI MAPYA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (Kulia) Dkt.Faisal H.H.Issa akiweka saini katika "MEMORANDUM OF UNDERSTANDING" kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kimataifa la Himo, kulia kwake ni Mwakilishi wa Benki ya TIB Bwana Allan Magoma.Waliosimama ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (katikati),kulia kwake Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe. Samwel  Sitta  na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe.Dkt Ibrahim Msengi wakishuhudia tukio hilo la kihistoria katika mkoa wa Kilimanjaro la tarehe 09/10/2012